Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA, shambulio hilo lilitokea Ijumaa jioni, ambapo mizinga ya Israel ililenga shule iliyopo katika kitongoji cha Al-Tuffah mashariki mwa Gaza, ambayo ilikuwa ikitumika kama kituo cha kuwahifadhi wakimbizi. Shambulio hilo lilisababisha kuuawa kwa Wapalestina 6 na kujeruhiwa kwa watu 5, huku hali ya baadhi ya majeruhi ikiripotiwa kuwa mbaya.
Vyanzo vya kitabibu vimesema kuwa miili ya mashahidi 6 — wakiwemo mwanamke mmoja - pamoja na majeruhi 5 (watu 3 wakiwa katika hali mbaya na 2 wakiwa na majeraha ya wastani) imepelekwa katika Hospitali ya Al-Maamadani katikati ya Gaza.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa tanki la Israel liliingia katika eneo hilo, likakaribia shule hiyo, kisha likapiga makombora kadhaa kuelekea kituo cha hifadhi, jambo lililosababisha vifo na majeruhi miongoni mwa raia wa Kipalestina. Aidha, wamesema kuwa vikosi vya Israel vilizuia kwa zaidi ya saa mbili timu za uokoaji na magari ya wagonjwa kufika eneo la tukio, hali iliyochelewesha kuhamishwa kwa waathirika.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao, shambulio hilo lilifanyika wakati wa kuendelea kwa hafla ya harusi, jambo lililoongeza idadi ya waathirika. Eneo lililolengwa ni miongoni mwa maeneo ambayo jeshi la Israel lilikuwa limejiondoa awali kwa mujibu wa makubaliano ya usitishaji vita.
Ikumbukwe kuwa vita vya uharibifu vya Israel dhidi ya Gaza, vilivyoanza tarehe 8 Oktoba 2023 na kuendelea kwa miaka miwili kwa uungwaji mkono wa Marekani, vimesababisha zaidi ya mashahidi 70,000 na majeruhi 171,000, ambapo walio wengi ni wanawake na watoto. Vita hivyo pia vimesababisha uharibifu mkubwa, huku Umoja wa Mataifa ukikadiria gharama ya ujenzi upya kufikia dola bilioni 70.
20 Desemba 2025 - 19:46
News ID: 1764063
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeua mashahidi 6 Wapalestina na kuwajeruhi watu 5 wengine, baada ya kulipua kwa mizinga kituo cha hifadhi kilichopo mashariki mwa Jiji la Gaza, wakati wa hafla ya harusi.
Your Comment